Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 21, 2024 Local time: 19:43

Mapigano mapya Somalia yaua 17


Mashahidi huko Somalia wanasema watu 17 wameuwawa katika mapigano mapya kati ya wanamgambo wa ki-Islam na majeshi ya serikali. Wakazi wa Yeed, mji uliopo kwenye mpaka Somalia na Ethiopia wanasema wapiganaji kutoka kundi la uasi la al-Shabab waliwavamia wanajeshi wa serikali siku ya Jumapili.

Pande zote mbili zilidai ushindi kwenye mapigano hayo na haikuweza kufahamika nani anayeudhibiti mji huo leo. Inasemekana wengi wa waliokufa walikuwa wapiganaji. Kundi la al-Shabab na washirika wake Hizbul Islam wamekuwa kwenye mapigano tangu mwanzoni mwa mwezi Mei. Makundi hayo yanajaribu kuiangusha serikali ya Somalia na kuiweka nchi katika taifa la ki-Islam.

Watu 21 waliuwawa wakati wauaji wa kujitoa mhanga wa kundi la al-Shabab walipovamia kituo cha walinda amani cha umoja wa Afrika katika mji mkuu Mogadishu siku ya Alhamisi. Mjumbe maalumuwa umoja wa Afrika huko Somalia aliomba silaha zaidi kwa ajili ya serikali ya Somalia. Wanajeshi 4,000 wa umoja wa Afrika kutoka Uganda na Burundi wanaisaidia serikali kudhibiti miji mikuu yakiwemo maeneo makuu yabandari na uwanja wa ndege.

XS
SM
MD
LG