Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 21, 2023 Local time: 08:50

Usalama unaimarishwa Laikipia Kenya


Hali ya wasiwasi bado imetanda katika maeneo ya kaskazini mwa Kenya kufuatia mauaji ya watu wasiopungua 32, waliouwawa wakati majambazi kutoka eneo la Pokot walipowashambulia wakazi wa eneo la Samburu na kuiba mifugo yao.

Kufuatia tukio hilo serikali imeimarisha usalama kwa kupeleka polisi zaidi katika eneo hilo, ikiwa ni juhudi za kuzuia ghasia zaidi na kuhakikisha walioibiwa mifugo yao wamerudishiwa.

Duru za maafisa wa polisi katika maeneo hayo zinasema, uvamizi huo ulifanywa na zaidi ya majambazi 150 waliokuwa na lengo la kuiba zaidi ya ng’ombe elfu kumi kutoka jamii ya wasamburu.

Miongoni mwa watu waliouwawa kwenye tukio hilo ni pamoja na wanawake watatu na watoto nane, watu kumi na mbili walijeruhiwa vibaya kwenye shambulizi hilo na baadhi yao walipelekwa mjini Nairobi kwa matibabu zaidi huku watatu kati yao wakiwa mahututi.

Miezi michache iliyotopita viongozi wa eneo hilo walilalamikia serikali kuhusu ukosefu wa usalama na hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa na serikali.

XS
SM
MD
LG