Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 16:58

Madhehebu ya Kikristo yagawanyika kuhusu waraka wa Uchaguzi


Madhehebu ya dini za kikristo nchini Tanzania yanavutana juu ya waraka uliotolewa na kanisa katoliki nchini Tanzania kuhusu kuelimisha waumini wake kumchagua kiongozi anayefaa katika uchaguzi ujao mwaka 2010.

Hivi karibuni Askofu msaidizi wa kanisa katoliki , jimbo kuu la Dar es salaam ,mhashamu Methodius Kilaini alinukuliwa na vyombo vya habari akitetea waraka uliotolewa na kanisa hilo wa kupinga viongozi mafisadi ambao ulitoa changamoto kwa viongozi wa kiislamu kutoa waraka wake unaodai kuwaelimisha waumini wake kuelekea kipindi cha uchaguzi.

Pamoja na waraka huo wa kanisa katoliki kuungwa mkono na madhehebu mengine ya kikristo, lakini kuna baadhi ya mengine yaliyoupinga na kudai unaweza kuleta mgawanyiko kwa wananchi kwa sababu umejaa ushawishi wa kisiasa.

Miongoni mwa madhehebu hayo ni pamoja kanisa la Askofu mkuu wa Full Gospel Bible Fellowship –FGBF, Zakary Kakobe, aliyepinga waraka huo akisema kuwa unashambulia viongozi kuhusu ufisadi na hauna nidhamu kwa rais wa nchi.

Naye katibu mkuu wa ushirika wa kipentekoste Bishop David Mwasota na mchungaji Christopher Mtikila kiongozi wa chama cha siasa cha DP nchini Tanzania walipoulizwa maoni yao na Sauti ya Amerika kuhusu waraka huo, waliyasihi madhehebu yote ya dini za kikristo kuungana na kuupokea waraka huo wenye malengo mazuri kwa Tanzania na watu wake.

Askofu Mwasota alisema wakristo hawana budi kuiga mfano wa waislamu katika kauli mbiu ya kuelimisha waumini wake kumchagua kiongozi aliyebora katika uchaguzi wa mwaka 2010.

XS
SM
MD
LG