Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 21, 2024 Local time: 08:38

Wanajeshi waandamana Afrika Kusini


Serikali ya Afrika Kusini inasema polisi watachukua hatua kali dhidi ya maandamano ambayo yatageuka kuwa ya uharibifu. Onyo hilo limekuja siku moja baada ya polisi kutumia gesi ya machozi kutawanya zaidi ya wanajeshi elfu moja waliokuwa wakijaribu kuingia katika majengo ya Union, ambayo ni makazi rasmi ya Serikali ya Afrika Kusini huko Pretoria. Magari kadhaa yaliharibiwa wakati wa tukio hilo. Wanajeshi walikuwa wakidai nyongeza ya mishahara kwa asilimia 30. Msemaji Themba Maseko alisema baraza la mawaziri limelaani maandamano hayo, ambayo alisema yamefanya uharibifu mkubwa wa hadhi kwa nchi ambayo ni thabiti na yenye demokrasia changa.

XS
SM
MD
LG