Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 15, 2024 Local time: 07:22

Mashirika ya Dini Tanzania Yatoa Ilani ya Uchaguzi.


Na waandishi wetu.

Vuguvugu la uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 nchini Tanzania linazidi kupamba moto huku baadhi ya madhehebu ya dini yakijiingiza katika kile wanachoelezea kuwa kuwaelimisha waumini wa Tanzania kwa ujumla umuhimu wa kushiriki uchaguzi huo na aina ya viongozi wa kuwachagua.

Miongoni mwa madhehebu hayo nikanisa Katoliki na waumini wa dini ya Kiislam ambayo kwa nyakati tofauti wameandaa waraka unaotoa mwongozo unaohusiana na uchaguzi huo mkuu. Waumini wa dini ya Kiislam nchini Tanzania wametangaza azma yao ya kuzindua waraka unaoelekeza aina za viongozi wa kuwachaguakwenye uchaguzi huo.

Akizungumza na sauti ya Amerika kiongozi wa dini ya Kiislam sheikh Ponda Issa Ponda amesema muongozo wa dini hiyo ya Kiislam unalengo la kuwaelekeza wananchi kuweza kupiga kura kama kundi maslahi tofauti na ule mwongozo wa Katoliki wenye lengo na madhumuni makubwa ya kisiasa.

Naye Askofu msaidizi wa jimbo kuu la Katoliki jijini Dar-es-salaam, Methobius Kilaini amesema tangu kuanzishwa vyama vingi kanisa hilo limekuwa likitoa mwongozo wa kuwaelekeza watu wote na kuhamasisha nchi nzimakuelewa mfumo wa chama kimoja kuingia vyama vingi, ikiwa ni pamoja na kupiga kura, kugombea na ulazima wa kuchagua viongozi bora.

XS
SM
MD
LG