Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 01:07

Dunia yaomboleza kifo cha Kennedy.


Na waandishi wetu

Wanasiasa na wananchi wa kawaida sehemu mbali mbali duniani wanaomboleza kifo cha mwanasiasa wa Marekani Edward Kennedy ambaye alikuwa mmoja wa maseneta wa muda mrefu katika historia ya Marekani. Kennedy, alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 77. Alikuwa mdogo wa marehemu rais wa zamani John F. Kennedy.

Katika taarifa familia imemwelezea Seneta Kennedy kama kiini cha familia ambacho hakiwezi kuzibika na nuru katika maisha. Anatarajiwa kuzikwa katika makaburi ya kitaifa ya Arlington sehemu ya mwisho ya mapumziko waliyozikwa kaka zake rais wa zamani wa Marekani John F. Kennedy na Seneta wa zamani Robert Kennedy .

Katika rambirambi zake rais wa Marekani Barack Obama alieleza kuvunjika moyo kwake kufuatia kifo cha Kennedy. Bwana Obama alimwelezea Kennedy kama kiongozi shupavu na mpigania haki za wanyonge ambaye atakumbukwa daima.

Katika kipindi chake cha useneti alikuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha sheria inapitishwa kuhusu haki za wafanyakazi , ufadhili wa elimu, sera za mambo ya nje, sera za huduma ya afyana sheria ya uhamiaji.

Sauti ya Amerika ilizungumza na wachambuzi wa masuala ya kisiasa juu ya kifo cha Seneta Kennedy akiwemo Katibu Mkuu wa zamani wa OAU Salim Ahmed Salim, mbunge wa Kenya Ababu Namwamba, mhadhiri Prof. Charles Bwenge, mhadhiri John Maina na mwandishi wa habari wa Afrika Kusini Issa Khomo .

XS
SM
MD
LG