Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Julai 24, 2024 Local time: 21:12

Ted Kennedy - mwanasiasa mkongwe mashuhuri afariki dunia


Seneta Edward Kennedy wa jimbo la Massachusetts, mzee wa mwisho kutoka familia yenye ushawishi mkubwa wa kisiasa nchini Marekani, alifariki jumanne usiku kutokana na saratani ya ubongo akiwa na umri wa miaka 77.

Taarifa iliyotolewa na familia ya Kennedy inaeleza kuwa seneta huyo wa chama cha Democratic alifariki nyumbani kwake katika mji wa Hyannis Port. Taarifa inamuelezea kama "kiongozi wa familia ambae nafasi yake haiwezi kuchukuliwa na mwingine na ni mwenge wa furaha machoni mwetu"

Kennedy hakuwa anahudhuria vikao vya bunge takriban mwaka huu wote kutokana na ugonjwa wake, uliomlazimisha kufanya kazi kutoka nyumbani kwake, akitetea suala muhimu alilokuwa akilishughulikia maisha yake yote, mageuzi ya huduma za afya.

Mwezi Januari, seneta huyo alizirai katika ukumbi mkuu wa bunge baada ya kuapishwa Rais Barack Obama, ambaye alimuunga mkono tangu mwanzoni mwa kampeni yake ya kupigania kiti cha rais 2008.

Rais Obama hivi karibuni alimpatia Kennedy aliyekua akiugua, nishani ya Uhuru ya rais.

Kennedy, aliliwakilisha jimbo la Massachusetts katika baraza la Seneti la Marekani tangu 1962, alipochaguliwa kuchukua kiti kilichokua kinashikiliwa na kaka yake mkubwa, Rais John F. Kennedy. Wakati wa muda wake wote bungeni alikua mtetezi mkuu wa wanyonge, akiongoza maslahi ya waliberali, ikiwa ni pamoja na kutetea haki za kiraia, elimu na uhamiaji, ukiongeza huduma za afya.

Alikuwa mpinzani mkuu wa vita vyote, vya Vietnam na uvamizi wa Marekani Irak 2003.

Ameacha mke, Victoria Reggie, pamoja na watoto wake wa tatu kutokana na ndoa yake ya kwanza ya miaka 25 na Joan Bennett Kennedy, pamoja na mabinamu wengi. Kitabu juu ya maisha yake kinatazamiwa kuchapishwa mwakani.

XS
SM
MD
LG