Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 06, 2024 Local time: 11:36

Kenya imeanza zowezi lenye utata la kuhesabu watu wake


Kenya imeanza zoezi la kuhesabu watu kote nchini, huku kukiwa na tuhuma za ukabila na ukosefu wa usalama. Idadi ya hesabu ya watu inatarajiwa kuonyesha ongezeko la idadi kamili ya watu nchini humo ambayo tayari inaathiriwa na ukosefu wa rasimalia za msingi.

Inakadiriwa kuwa idadi ya watu imeongezeka kwa milioni kumi nchini Kenya, tangu kufanyika kwa sensa ya mwisho muongo mmoja uliopita, na kuifanya idadi ya watu nchini humo kufikia milioni 40.

Ongezeko la idadi ya watu nchini humo ni sababu ya kuwa na khofu ndani ya nchi. Wataalamu wanasema hali ya chakula nchini, maji na ugavi wa nishati viko katika viwango vya dharura, kutokana na ukame wa muda mrefu ulioikumba nchi na kwa upande mwingine kutokana na utawala mbaya wa rasimali za asili.

Lakini utaratibu wa kufanya zoezi la sensa nchini Kenya umekuwa na matatizo katika nchi ambayo maeneo ya mijini yameelezewa kuwa ni sekta zisizo rasmi za makazi na ambapo maeneo ya vijijini mara kwa mara yanakuwa na idadi kubwa ya watu wa jamii ya wafugaji wanaohama hama.

Mbali na vikwazo katika zoezi hili kuna suala la uhamaji ambalo limetokea kwasababu ya ukame mkubwa ambao umewalazimisha wafugaji kwenda katika nchi jirani kama vile

Uganda na Sudan. Serikali imejihusisha na jamii kuwafikia watu hao na pia kuahidi msaada wa chakula ikiwa ni moja ya juhudi za kuwafanya wahamaji warejee maeneo ya mpakani ili wahesabiwe.

Rais ametangaza Jumanne ni sikukuu ya kitaifa ili watu waweze kubaki nyumbani wakati wa zoezi hilo.

Wakati huo huo kiongozi wa kina mama kutoka Kisauni, Mombasa, Bi Afia Rama alizungumzia kuhusu zoezi hili na kuelezea baadhi ya maswali ambayo yako katika fomu za sensa ambayo yamewakera baadhi ya watu.

Zinazohusiana

XS
SM
MD
LG