Rais wa Marekani Barack Obama na mgeni wake Rais wa Misri, Hosni Mubarak wameelezea imani kuhusu uwezekano wa kusonga mbele kwa utaratibu wa amani wa waisrael na wapalestina. Rais Obama aliwaambia waandaishi wa habari huko White House leo Jumanne kwamba kumekuwepo na harakati katika mwelekeo sahihi. Alikuwa akijibu swali kuhusu ripoti kwamba Israel kimya kimya haitaki kusitisha mradi wa ujenzi wa nyumba mpya huko Ukingo wa Magharibi. Bwana Obama pia alielezea kuhusu kuondolewa kwa baadhi ya vizuizi huko Ukingo wa Magharibi na kuboresha majeshi ya usalama ya wapalestina.