Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 09, 2023 Local time: 15:23

Benki za Nigeria zapewa msaada wa fedha


Benki Kuu ya Nigeria inasema itazipa benki zenye matatizo nchini humo zaidi ya dola bilioni mbili na nusu ikiwa ni mpango wa kwanza wa kuziokoa benki hizo tangu kuanza kwa mzozo wa fedha ulimwenguni. Mkuu wa Benki Kuu, Lamido Sanusi pia alisema kuwa serikali itawaondoa watendaji wakuu katika benki tano. Alisema serikali haitaruhusu benki yoyote kushindwa na inatoa dhamana kwa watoa mikopo na wale wataoweka fedha zao. Sanusi alisema serikali haina mpango wa kutaifisha mabenki yatakayopatiwa msaada. Alisema Benki Kuu inataka mabenki yenye matatizo kujiweka katika hali nzuri na kurejesha fedha walizokopeshwa na serikali.

XS
SM
MD
LG