Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 24, 2024 Local time: 08:34

Clinton akamilisha ziara yake barani Afrika


Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Hillary Clinton amehitimisha ziara ya siku 11 barani afrika kwa kusema ana imani kuhusu hali ya baadae ya bara hilo, lakini hatapuuza matatizo yao. Katika mkutano na waandishi wa habari huko Cape Verde, ikiwa ni kituo chake cha mwisho barani Afrika leo Ijumaa, Clinton alisema kwamba hasikitishwi kwa kile alichokiita, ‘ujumbe mkali’ aliowapa viongozi wa bara hilo. Alisema utawala wa Obama hautajiweka kando na matatizo ya Afrika na unataka kuwasaidia waafrika kubadili mwelekeo wa nchi zao.

XS
SM
MD
LG