Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 15, 2024 Local time: 03:39

Majeshi ya Marekani  Afghanistan ya wafurusha Taliban


Msemaji wa wizara ya ulinzi ya Marekani Pentagon, amesema kutakuwepo na mashambulizi zaidi sawa na lililoanzishwa Jumatano huko kusini mwa Afghanistan ili kuchukua tena udhibiti wa wilaya ilyokua inashikiliwa na Taliban kwa muda mrefu katika jimbo la Helmand.

Msemaji wa wizara ya ulinzi Bryn Whitman amesema, operesheni katika wilaya ya Nawzad ilipangwa ili kuwafyeka waasi kutoka eneo hilo kabla ya uchaguzi wa rais wa Afghanistan, siku ya Alhamisi ijayo.

"Vikosi vya Marekani pamoja na washirika wao wa Afghanistan na wanajeshi wengine wa ushirika wamekwenda huko kujaribu kuhakikisha kwamba wakati uchaguzi unapokaribia wa Afghan wataweza kua na uhuru wa kutembea na kwenda kupiga kura katika vituo vya kura, na kufanya hivyo katika hali ya usalama bila ya kuzuiliwa." Alisema "operesheni kama hii inachangia kufikia lengo hilo."

Whitman alisema kutakua na mashambuliyo zaidi mnamo siku zinazokuja lakini hayatasita baada ya uchaguzi.

XS
SM
MD
LG