Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 04, 2022 Local time: 14:05

Clinton atoa wito wa uchaguzi wa rais Angola


Bi Hillary Clinton alisema ukuaji wa uchumi huko Angola, unategemea utawala bora na taasisi madhubuti za kidemokrasia. Baada ya kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola, Assuncao Afonso Dos Anjos, Waziri Clinton alisema ana matumaini kwamba uchaguzi wa kwanza wa rais nchini humo, katika kipindi cha miaka ishirini, utafanyika kwa wakati unaofaa.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola, Bw. Dos Anjos alisema, uchaguzi wa rais ulitarajiwa kufanyika baadae mwaka huu, huenda ukakhirishwa hadi mwaka wa 2010, ili kuiwezesha Angola kupitisha katiba mpya. Aliongezea kusema kwamba, Angola ilikosolewa kwa kuchelewesha uchaguzi wa bunge, ambao hatimaye ulifanyika mwaka jana, na kwamba sasa wanomba muda zaidi ili kuandaa uchaguzi wa rais.

Ni miaka 7 tu, tangu Angola isitishe vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa kipindi cha miaka 27, vita ambavyo serikali ya Marekani iliwasaidia waasi wa kundi la UNITA. Kundi hilo hivi sasa, ndilo kundi kuu la upinzani, na ambalo linadai kwamba Rais Jose Eduardo Dos Santos anachelewesha uchaguzi kusudi, ili kuongeza muda wake mamlakani.

Angola na Nigeria ndio mataifa makuu barani Afrika yanayozalisha mafuta ghafi, na mashirika ya kimarekani ndiyo yanayo simamia takriban nusu ya uzalishaji wa mafuta hayo nchini Angola. Suala la mafuta ni sehemu kubwa kabisa katika ziara ya Bi clinton, hasa alipokutana na Waziri wa mMafuta wa Angola, na kushuhudia kutiwa saini mkataba baina ya shirika la Chevron, na shirika la Marekani la maendeleo ya kimataifa, na serikali ya Angola, ili kusaidia miradi ya kilimo.
Japo Angola ina utajiri mkubwa wa mafuta, theluthi mbili ya wananchi wanaishi kwa kipato cha chini ya dola mbili kwa siku. Nchi hiyo ya Angola iko nambari 158 katika orodha ya nchi 180 zenye kuongoza katika ulaji rushwa, kama ilivyo chunguzwa na shirika linoshoghulikia ulaji rushwa la Transperency International.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani aliisifu Angola kwa upande mwingine kwa kuchukua hatua za kupambana na ulaji rushwa katika sekta ya mafuta, kwa kuchapisha mapato yake kwenye mtandao na kwa kufanya kazi kwa ushirikiano na maafisa wa kimarekani kuzidisha uwazi.

Alisema ulaji rushwa unapunguza imani ya watu kwa mfumo wa demokrasia, kadhalika, kupotosha utawala bora na kuzuia watu kuhusika kikamilifu katika jamii zao.

Alipoulizwa kuhusu ukuaji wa ushawishi wa China huko Angola, na mikopo ya zaidi ya dola bilioni 5, ya China kwa serikali ya Luanda, Bi Clinton alijibu, kwamba, yeye hatazami shughuli za watu wengine huko Angola, lakini anachotazama ni mambo gani Marekani inaweza kufanya ili kuboresha na kuendeleza uhusiano baina ya cnhi hizo mbili.

Ziara hiyo nchini Angola, ni kituo cha tatu cha ziara yake barani Afrika, hivi sasa anatarajiwa kutemebelea Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo, kabla kuelekea nchini Nigeria, Liberia na visiwa vya Cape Verde.

XS
SM
MD
LG