Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 27, 2020 Local time: 12:46

Rais Kabila afukuza kazi watumishi wa serikaliRais Joseph Kabila wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo amewafukuza kazi wakuu 80 wa mashirika ya umma na maafisa wa vyeo vya juu serikalini, kwa tuhuma za ulaji rushwa.

Mwandishi wa Sauti ya Amerika huko Kinshasa anaripoti kwamba maafisa hao wameondolewa kazini kutokana na tuhuma za rushwa, uongozi mbaya na matumizi mabaya ya mali za umma.

Vile vile Rais Kabila ameamuru kustaafishwa kwa wafanyakazi 1200 wa serikali ambao walishatimiza umri wa kustaafu ama wamefanya kazi zaidi ya miaka 35.

Hatua hiyo ya Rais Kabila ni kampeni yake ya kupambana na rushwa aliyoianza wiki mbili zilizopita ambapo aliwaachisha kazi mahakimu kadhaa wakiwemo Mwanasheria Mkuu na kiongozi wa Mahakama Kuu nchini humo.

Kura ya Maoni : Uchaguzi Tanzania

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

XS
SM
MD
LG