Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 09:19

Marekani kuisaidia Serikali ya Somalia


Serikali ya Rais Barack Obama imeeleza bayana kwamba iko tayari kuisaidia Serikali ya Somalia kujilinda kutokana na mashambulizi ya waasi wa Kiislamu wenye kutuhumiwa kuwa na uhusiano na al-Qaida.

Akizungumza na wandishi habari siku ya alhamisi, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje anaeshughulika na masuala ya Afrika Johnnie Carson, alitangaza ziara ya mataifa saba ya Afrika itakayofanywa na Waziri wa Mambo ya Nje Bi Hillary Clinton kuanzia wiki ijayo.

Bw Carson alisema Waziri wa Mambo ya Nje atakutana na Rais wa Serikali ya mpito ya Somalia mjini Nairobi, ambako atakutana pia na viongozi wa vyama vyote vikuu vya siasa kenya katika serikali ya umoja wa kitaifa, na kuhudhuria mkutano wa kuimarisha biashara kati ya Marekani na Africa AGOA.

Bi Clinton pia atazitembelea Afrika Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Nigeria, Liberia, na visiwa vya Cape Verde, ikiwa ni ziara ya kuendeleza ujumbe wa Rais Obama alioutoa mapema mwezi huu huko Ghana. Ujumbe huo ulihusu msaada wa Marekani kwa utaratibu wa kidemokrasia barani Afrika, ukuaji wa kiuchumi na juhudi za kutanzua migogoro.

XS
SM
MD
LG