Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Septemba 26, 2022 Local time: 21:51

Marekani inaongeza juhudi za kupatikana amani  Mashariki ya Kati


Akizungumza mjini Amman, Jordan baada ya kuwa na mazungumzo na mfalme Abdullah, Waziri wa Ulinzi wa Marekani Robert Gates,alionya Iran kwamba Marekani itahimiza kuchukuliwa vikwazo vikali zaidi, ikiwa serikali ya Tehran haitojibu pendekezo la serikali ya Washington kujadili suala la mpango wa nyuklia wa Iran.

Mapema Jumatatu, Bw Gates alikuwa mjini Jerusalem ambako alizungumzia juu ya nia yampango wa nyuklia wa Iran na waziri mwenzake wa Israel, Ehud Barak. Bw Barak alisema, Israel haiondoi uwezekano wa hatua ya aina yeyote kuchukuliwa kuhusiana na mpango wa nyuklia wa Iran, lakini alisema kipaumbele kinabaki kuwa diplomasia. Bw Gates alikutana pia na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.

Wakati huo huo mjumbe maalum wa Marekani kwa ajili ya Mashariki ya Kati George Mitchell alikuwa huko Israel na kukutana na rais Shimon Peres siku ya Jumatatu. Hapo tena alisafiri hadi Ukingo wa Magharibi kwa mazungumzo na rais wa mamlaka ya Wapalestina Mahamoud Abbas, na mpatanishi mkuu wa Abbas, Saeb Erekat.

Mjumbe huyo alizungumzia wito wa Marekani wa kusitishwa ujenzi wa makazi ya walowezi wa kiyahudi,pamoja na viongozi hao wawili.

Kabla ya hapo asubuhi ya Jumatatu Bw. Mitchell alikutana na rais Hosni Mubarak wa Misri, mjini Cairo.

XS
SM
MD
LG