Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 21:41

Rais Kikwete azindua mkonga wa mawasiliano


Serikali ya Tanzania imezindua rasmi mkonga wa mawasiliano ambao unajulikana kama fiber-optic ambao hupitishwa chini ya bahari. Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete alikuwa mgeni wa hesima katika uzinduzi huo na kuelezea kuwa nchi ambazo mkonga huo unapitia zitakuwa na fursa ya kupiga hatua kubwa katika sekta ya mawasiliano.

Rais Kikwete amesema mkonga huo utasaidia kuharakisha shughuli za maendeleo katika eneo zima la Afrika Mashariki. Alielezea jinsi Tanzania itakavyoweza kufaidika katika soko la ndani kwa kuunganishwa na upande wa pili wa dunia, hatua ambayo alifafanua kwamba itawasaidia wasomi wapya kaitka vyuo vikuu na hivyo kuharakisha ukuaji wa huduma nyingine zinazofanikishwa kwa kutumia mtandao wa mawasiliano.

Baadhi ya nchi ambazo mkonga huu wa fiber-optic umepitia ni pamoja na Afrika Kusini, Msumbiji, Misri na kupitia barani Ulaya na hali kadhalika nchini India.

XS
SM
MD
LG