Maafisa wa Sudan Kaskazini na Kusini wanasema wataheshimu maamuzi ambayo yanabadili mipaka katika mkoa wenye mzozo wa Abyei. Mahakama ya Kudumu ya Usuluhishi huko The Hague ilibadili eneo la mipaka upande wa mashariki na magharibi katika mkoa wenye utajiri wa mafuta. Maamuzi hayo yalitolewa jana. Uamuzi huo unapunguza ukubwa wa abyei na sehemu kubwa inayotoa mafuta iko kwenye serikali ya Sudan upande wa Kaskazini. Maafisa wa Kusini wameelezea kusikitishwa na maamuzi hayo lakini wanasema watayakubali.