Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Septemba 28, 2022 Local time: 11:37

Biashara ya madini ya chochea zaidi vita DRC


Ripoti mpya iliyotolewa kuhusiana na biashara ya madini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na shirika la Global Witness, shirika linalofuatilia jinsi biashara ya kimataifa inavyoathiri mapigano ya wenyewe kwa wenyewe na kuchangia katika ukosefu wa utulivu katika sehemu mbali mbali za dunia.
Kufuatana na shirika hilo, kutolewa fedha kwa njia zisizo za moja kwa moja kwa makundi yenye silaha katika eneo hilo la Afrika ya Kati kupitia shughuli za biashara za makampuni ya kigeni, hazifuatiliwi kamwe na mataifa yanakotoka makampuni hayo ikiwa ni pamoja na Uingereza, Ubelgiji, Thailand Malaysia na Rashia.
Mkuu wa utafiti wa migogoro na rasil-mali katika shirika la Global Witness Mike Davis anasema, kuendelea hali ya kutochukuliwa hatua na baadhi ya nchi hizi ni jambo lizsilo kubalika, ukichukulia kuendelea mateso na ukiukaji wa haki za binadam biashara ya madini inasaidia kuendeleza.
Bw Davis anasema “tunadhani kwa hakika ni aibu sana kwa sababu ni zile zile serekali kama vile Uingereza zinazozungumzia juu ya kiwango cha misaada wanayotowa kwa kanda hiyo, lakini juhudi hizo kubwa zina kua hazina maana kutokana na shuguli mbaya za kampuni zao wenye na hii inapelekea hali isiyokubalika kabisa na ni unafiki mtupu.”
XS
SM
MD
LG