Mkutano maalum wa baraza la mawaziri huko Kenya umeahisirhwa kwa wiki moja baada malumbano makali kutokea kati ya wafuasi wa Rais Mwai Kibaki wa chama cha PNU na wale wa wazir mkuu Riala Odinga wa ODM.
Mawaziri hawakubaliani juu ya kuundwa kwa mahakama maalum ya kusikiliza kesi za wanaotuhumiwa kuhusika katika kupanga ghasia zilizotokea baada ya uchaguzi wa rais mapema mwaka jana.
Mawaziri wamepewa wiki moja kutafakari ikiwa kesi hizo zisikilizwe na mahakama maalum, au zipelekwe mbele ya mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC huko The Hague.
Mvutano huo umetatanishwa zaidi, kutokana na hatua iliyochukuliwa na tume ya taifa ya Haki za Binadam kutaja hadharani majina ya mawaziri, wabunge na baadhi ya wafanya bishara mashuhuri wanaoshukiwa kuhusika na ghasia hizo au kuwafadhili vijana walohusika na mauwaji hayo moja kwa moja.
Chama cha Odinga, ODM kimeanza kulalamika vikali kwamba majina mengi yaliyotajwa na tume hiyo ya haki za binadamu ni wafuasi wa chama chake. na katika hatua za kuwatuliza wafuasi wake kiongozi wa chama cha ODM, Bw Odinga aliwataka kutokua na wasi wasi. Bw Odinga anasema, "kama huna hatia inabidi kusimama imara, hapana kubabaika hapa na hapa eti leo oh The Hague leo, kesho ni hapa, kesho sijui Truth and Justice Reconciliation hapana".
Bw Odinga anadai kwamba wafuasi wake ndiyo walodhulumiwa zaidi na ghasia hizo. Lakini kuna baadhi kama waziri wa utali Najib Balala, anadai jina lake kwenye kundi la mawaziri walohusika na ghasia hizo kwa njia ya uchochezi.