Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 01, 2022 Local time: 16:52

Kibaki ahimiza uhusiano mzuri na Tanzania


Akiendelea na ziara yake ya kiserekali huko Tanzania, rais Mwai Kibaki wa Kenya alifungua siku ya alhamisi jengo jipya la ubalozi wa Kenya jijini Dar es laaam, ambalo amesema limefungua ukurasa mwingine wa mahusiano baina ya nchi hizo mbili.

Licha ya Kenya kujenga jengo hilo la ghrofa moja lililopo eneo muhimu la Oysterbay jijini Dar es salaam , Tanzania nayo inatarajia kuanza ujenzi wa jengo lake la ubalozi nchini Kenya baada ya kupewa eneo muhimu la ujenzi jijini Nairobi.

Katika hotuba yake rais Kibaki alizisihi nchi hizi mbili kuacha vijimaneno vya hapa na pale na kuendeleza historia ya mahusiano mema baina yao. Akizungumzia umuhimu wa bara la Afrika kujikomboa kiuchumi rais huyo wa Kenya alisisitiza muungano wa Afrika Mashariki baada ya sasa kuongezwa nchi za Rwanda na Burundi katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Kwa upande wake rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete hakusita kuonesha hisia zake kwa kusema kuwa katika ziara hiyo ya kirafiki viongozi hao wamezungumza mambo mengi na kukubaliana kuyafanyika kazi kwa pamoja.

XS
SM
MD
LG