Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 04:49

Mabalozi wahimiza Kenya kuunda Mahakama Maalum


Mabalozi wa nchi za Ulaya nchini Kenya alhamisi walitoa taarifa kali ya kuihimiza serikali ya nchi hiyo kubuni mahakama maalumu ya kuwashitaki watuhumiwa wa ghasia na mauaji yaliyotokea baada ya uchaguzi mkuu uliopita.

Wakiwahutubia waandishi wa habari mjini Nairobi mabalozi hao walihimiza serikali kubuni jopo maalumu la kisheria kuwashitaki watuhumiwa wa ghasia na mauaji yaliyofanyika nchini Kenya baada ya uchaguzi mkuu kufanyika. Pia wamehimiza bunge la taifa kuharakisha kubuniwa kwa jopo hilo.

Wakiongozwa na balozi wa Uswizi nchini Kenya Bibi Anna Brant mabalozi hao wamesema kuwa chaguo la mahakama ya The Hague lastahili kuwa chaguo la mwisho, iwapo serikali itashindwa kuafikiana kuhusu suala hilo.

Wito huo wa mataifa ya Ulaya umetolewa siku moja tu baada ya rais Mwai Kibaki na Waziri Mkuu Raila Odinga pamoja na baraza lote la mawaziri kuhitilafiana kuhusu suala hilo.

XS
SM
MD
LG