Mugani Desire, mwana muziki mashuhuri wa Burundi akifahamika zaidi kama Big Fariaz, ni mtindo wa muziki ambao vijana zaidi wanaeleza juu ya maisha wanaoishi katika vitongoji vya miji mikubwa na wala si muziki wa uhuni.
Akitembelea studio za VOA na kushiriki katika kipindi cha Muziki Kutoka Afrika anasema alianza kuimba akiwa na umri wa miaka 11 akikulia katika vitongoji muhimu vya Bujumbura, na kucheza na makundi kama Best Boys, Full Force na kadhalika.
Alisema wakati huo katika miaka ya 1990 muziki ulokua unawika ni ule wa MC Hammer, mropokaji mashuhuri wa Marekani, na ndiyo muziki ulomvutia zaidi. <Msani huyo anachukulia miongoni mwa waasisi wa muziki mtindo wa rap huko Burundi, kwani mwaka 1996 pamoja na wenzake Patrick na Dogg Dogg waliunda kundi la Nigga Soul, moja wapo ya makundi ya kwanza ya Hip Hop nchini humo.
Big Fariaz alihamia kenya baada ya kifo cha rafikia yake mkubwa Dogg, na huko kukutana na mwanamuziki mwengine mashuhuri wa Burundi Kidumu, anaemsifu kumsaidia kutoa nyimbo zake mashuhuri "Sitopenda tena", Uswazi, na Mbarira.
Kufuatia nyimbo hizo mwanamuziki huyo alianza kupata umashuhuri na tangu wakati huo kila kibao anachotoa kinaitikisa nchi. Hivi sasa Desire anaishi Ufaransa ambako anakundi lake wanajeshi, na anatarajia kutoa albamu mpya karibuni.