Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 31, 2023 Local time: 02:49

Tume ya Ukweli Burundi kuwashirikisha wananchi.


Serikali ya Burundi imeunda kamati ya watu sita ambayo itasimamia katika zoezi la kukusanya maoni ya wananchi kuhusu uundaji wa Tume ya Ukweli na Maridhiano. Tume hiyo ambayo itajishughulisha kusikiliza malalamiko na kuwahoji wale wanaoshutumiwa kutenda maovu wakati wa vita nchini humo inajumuisha wajumbe wawili kutoka serikalini, wajumbe wawili kutoka Umoja Mataifa na wajumbe wawili kutoka jumuia ya kiraia nchini humo.

Mmoja wa wajumbe katika kamati hiyo, Ndayizeye Joseph aliambia sauti ya Amerika kuwa zoezi la ukusanyaji litafanyika kwa mujibu wa maelekezo ambayo kamati hiyo imepewa na matokeo ya tume hiyo yatawasilishwa kwa Rais wa Burundi kwa ajili ya kuyafanyia maamuzi rasmi.

Bwana Ndayizeye amesema wananchi watakuwa na fursa ya kuelezea muundo na mfumo wa utendaji wa tume hiyo ili iweze kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.

XS
SM
MD
LG