Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Septemba 27, 2023 Local time: 22:18

AMISOM inasema hali si mbaya sana Somalia


Mwishoni mwa wiki jeshi la kulinda amani la Umoja wa Afrika AMISOM, huko Somalia, lililazimika kupambana na waasi wa kundi la Al-Shabab katika mapambano yaliyosababisha vifo vya watu 10 na wengine 120 kujeruhiwa.

Lakini hii leo msemaji wa AMISOM Meja Barigye Bahuko, anasema ghasia hizo haimanishi hali ni mbaya hata kutoweza kuingia Mogadishu. Alisema, "watu wa magazeti ndio (wanatia chumvi) mambo hapa na siyo namna inavyo sikika huko".

Msemaji huyo alisema ni kweli wapiganaji wa Al-Shabab wanasababisha tatizo lakini, mapigano yao ni yale ya hapa na pale, kushambulia halafu kukimbia. Anasema tatizo kubwa ni kwa sababu serekali ni mpya, hakuna tasisi thabiti za usalama, sheria na utawala ili kuweza kuwadhibiti waasi hao.

Meja Bahuko anasema AMISOM inajaribu kutoa mafunzo kwa wanajeshi na polisi wa serekali ili kuweza kukabiliana na wahalifu, baada ya zaidi ya miaka ishirini ya kutokuwepo na utawala na serekali kuu nchini humo.

Amesema Serekali ya mpito inahitaji msaada kuweza kudumisha tena amani katika nchi hiyo na inabidi kusiadiwa kwa kuunga mkono juhudi zao za kutafuta amani na upatanishi.

Zinazohusiana

XS
SM
MD
LG