Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 01, 2023 Local time: 17:51

Rais Obama alihutubia bunge la Ghana


Akilihutubia bunge la Ghana huko Accra, Rais Barack Obama alifafanua sera ya utawala wake kuelekea Africa. Aliwambia wabunge wa Ghana na wageni waloalikwa kwamba kuheshimiana ndiyo mzingi wa ushirikiano kati ya nchi yao na Marekani.

Kiongozi huyo wa marekani alisema utawala wake umenuia kutoa dola bilioni 63 kwa ajili ya miradi ya afya katika kupambana na malaria, polio, kifua kikuu na ukimwi barani Afrika.

Rais Obama alikua na maneno makali kuhusiana na migogoro barani humo akiielaza kua ni kitanzi kinachoibana Afrika. Alisema kumpinga mtu wa kabila au anamuamini mtume toifauti nawe ni jambo lisilo kubalika katika karne ya 21.

Aliwambia walohudhuria kikao hicho maalum kwamba mustakbali wa Afrika uko mikononi mwa wa-Afrika wenyewe.

Ziara hii ya kihistoria ya Rais Obama huko Ghana, ni ya kwanza kufanywa na rais wa Marekani mwenye asili ya kiafrika. Alisema alichagua Ghana kwa sababu ya jinsi demokrasia inavyo fanya kazi, na rais wake Jhon Atta Mills, ambae Bw Obama anasema ana nia ya dhati ya kupambana na ulaji rushwa.

Rais Obama na mkewe walizuru soko la zamani la biashara ya utumwa, Cape Coast Castle, ambako watiumwa wa kiafrika walikua wakisafirishwa kwa meli kuvuka bahari ya Atlantic kwa karibu miaka 300.

XS
SM
MD
LG