Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Februari 28, 2024 Local time: 16:25

Mamilioni wamuaga Michael


Familia, marafiki, na maelfu ya mashabiki na waloalikwa walitoa heshima zao za mwisho kwa mwimbaji mashuhuri Michael Jackson katika ukumbi mkubwa wa michezo huko Los Angeles, na sherehe zilizofanyika katika sehemu mbali mbali za dunia.

Sherehe za kumbukumbu zilifanyika Jumanne kwenye ukumbi wa Staples Center ambako Jackson alifanya mazoezi yake ya mwisho siku mbili kabla ya kufariki hapo June 25. Jeneza la rangi ya dhahabu lililopambwa na maua ya kuvutia liliwekwa mbele ya jukwaa.

Sherehe zilianza kwa mwimbaji mashuhuri Smokey Robinson kusoma risala kutoka marafiki wa mwimbaji huyo ikiwemo pia moja kutoka kwa rais wa zamani wa Afrika Kuisni Nelson Mandela.

Berry Gordy muanzilishi wa kampuni ya Motown Records, alisema Jackson alikua "kwa ufupi mtumbuizaji mkuu kuwahi kutokea."

Waimbaji na wasanii wengine wengi mashuhuri akiwemo Stevie Wonder, Lionel Richie, Brooke Shields waliimba au kutoa sifa zake.

Na kufikia karibu na mwisho, wasanii hao mashuhuri walisimama pamoja kwenye jukwaa na kuimba wimbo wa "We Are the World," nyimbo mashuhuri ya 1985 aliyoandika Jackson na Lionel Richie kuchangisha fedha kwa ajilia ya watu wanaokabiliwa na njaa Afrika.

Mbali na waliokua huko Staples Center, umati mkubwa wa watu ulikusanyika katika sehemu mbali mbali za Los Angeles na kwengineko duniani. Maafisa wa mji wa Los Angeles wanasema mashabiki waliowasili huko huwenda wakachangia hadi dola milioni 4 za matumizi kuweza kusaidia mji huo unaokumbwa na ukosefu mkubwa wa fedha.
XS
SM
MD
LG