Rais wa Sudan, Omar Hassan al Bashir atakuwepo katika mkutano huo
akikaidi hati ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu, waziri mkuu wa
Italy, Silivo Berlusconni na rais wa Brazil Lula da Silava pia wapo
kwenye orodha ya wageni. Lakini pengine habari kubwa ni kwamba rais wa
Misri, Hosni Mubarak huenda naye akajitokeza.
Kiongozi huyo wa
misri mwenye umri wa miaka 81 hajawahi kuhudhuria mkutano wa viongozi
wa Afrika tangu kuepuka jaribio la kuuawa katika mkutano wa umoja wa
nchi huru za afrika mwaka 1995 huko Addis Abeba.
Sauti ya
amerika imeshindwa kupata visa ya kuhudhuria mkutano huo, lakini
wanadiplomasia na waandishi wa habari walisema mkutano huo unafanyika
katika hali ya sherehe.
Mkutano wa mwisho wa umoja huo uliofanyika Feburary ulihudhiriwa na viongozi 21 na kumuona Muammar Gadhafi akiapishwa. Kuna wasi wasi kuhusu idadi ya watakaojitokeza huenda isiwe kubwa. Lakini bwana Gadhafi anazungumzia kuwasilisha pendekezo lake la kuundwa kwa Umoja wa Mataifa ya Afrika, wengi ambao waliodhaniwa hawatafika pengine huenda wakahudhuria.
Akizungumza na Sauti ya Amerika katibu mkuu wa zamani wa OAU Bw Salim Ahmed Salim, alisema mbali na masuala ya kujitegemea upande wa kilimo na Afrika kuweza kujilisha wenyewe na masuala ya kiuchumi, anamini suala kuu litakua Darfur na migogoro mingine ikiwa ni Somalia, DRC, Madagascar na kadhalika.
Waandishi
wa habari huko Sirte wanasema IGAD kundi linalojumisha nchi za Pembe na
Mashariki Afrika zitauomba mkutano kubadili jeshi dhaifu la Umoja wa
Afrika – AMISOM na kuwa jeshi lenye nguvu.
IGAD inajumuisha nchi
sita za afrika Mashariki ambazo zinasemekana kuangalia maamuzi ya
awali ya kwazuia majirani wa Somalia kupeleka wanajeshi katika kikosi
cha amisom. Ethiopia na kenya zinapakana na Somalia na zimekuwa
zikiombwa kuwa na jukumu kubwa kwa jirani yao Somalia.