Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 05, 2024 Local time: 04:13

Ajali ya ndege Comoros


Kiasi ya watu 152 wanahofiwa wamefariki kutokana na ajali ya ndege ya aina ya Airbus 310 ya shirika la ndege la Yemenia iliyoanguka kaskazini ya kisiwa cha Ngazija visiwani Comoros.

Maafisa wa usfiri huko Comoros wanasema, ndege ilijaribu kutua kiasi ya saa tisa usiku lakini kutokana na upepo mkali na gurudumu moja la ndege kutoweza kushuka rubani alilazimika kuruka tena na hapo ndipo ajali ikatokea.

Mohamed Said Mchangama rais wa baraza la mameya wa Ngazija anasema hadi Jumanne usiku kulikua na hali ya mtafaruku kote nchini kwani kila mji kulikua na angalu mtu moja aliyekua abiria. Na hakuna aliyekua anajua kinachotendeka, hata hivyo ndege ya kijeshi ya Ufaransa ili kiwa na waokozi na madaktari imefika mchana wa leo na kuanza juhudi za kutafuta mili ya watu na mabaki ya ndege hiyo.

Familia ya wathiriwa wameimabia sauti ya Marekani kwamba hawana habari zezote juu ya juhudi zinazoendelea isipokua nambari imetolewa kupiga kujua habari za jamaa zao, lakini imekua vigumu kabisa kupata habari zozote.

XS
SM
MD
LG