Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 20:08

Kenya yadaiwa kukiuka haki za binadamu


Shirika la haki za binadamu la Human Rights Watch limeripoti kuwa majeshi ya Kenya ikiwa ni pamoja na idara ya Polisi yalihusika na ukiukaji wa haki za binadamu katika maeneo mbali mbali ya jimbo la kaskazini mashariki hasa katika eneo la Mandera na kwenye maeneo ya mpaka wa Kenya,Somalia na Ethiopia. Watu walioathirika zaidi na ukatili huo wa jeshi la Polisi ni raia wa Kenya wenye asili ya Kisomali zaidi ya watu 1200 walijeruhiwa vibaya sana na mtu mmoja kuuwawa. Pia wanawake wasiopungua 12 walibakwa na maafisa wa jeshi la Polisi. Kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu wa shirika hili la haki za binadamu ukatili ulifanywa na Polisi wakishirikiana na jeshi la nchi kavu walipokuwa katika heka heka za kuwasaka majambazi wenye silaha pamoja na wanamgambo wa kisomali wanaovuka mpaka na kuingia nchini Kenya. Hii si mara ya kwanza kwa mashirika ya haki za binadamu nchini humo kulaumu serikali ya nchi hiyo kwa kuhusika na ukatili na kukiuka haki za binadamu. Miezi kadhaa iliyopita mshauri wa umoja wa mataifa kuhusu haki za binadamu Profesa Phillip Alston alitoa ripoti kali kuhusu ukiukaji wa haki za binadamu nchini Kenya na akapendekeza kuondolewa madarakani kwa kamishna mkuu wa Polisi nchini Kenya Meja Jenerali Hussein Ali pamoja na mwanasheria mkuu wa nchi hiyo Bw. Amos Wacko.

XS
SM
MD
LG