Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 24, 2024 Local time: 09:08

Profesa Haroub Othman azikwa  Zanzibar


Mhadhiri wa siku nyingi katika chuo kikuu cha Dar-es-salaam na mchambuzi wa masuala ya siasa Profesa Othman Haroub amezikwa leo huko Zanzibar. Mazishi ya Profesa Haroub yamehudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali ya mapinduzi Zanzibar na Tanzania bara, viongozi wa dini, wanasiasa, wafanyabiashara na wanazuoni. Abdulshakur abood amezungumza na mwandishi wa habari Salim Said Salim kutoka Zanzibar ambaye alielezea mazishi ya mhadhiri huyo aliyefariki Jumamosi usiku nyumbani kwake Unguja akiwa na umri wa miaka 66. Alisema jopo la wanasheria Zanzibar walieleza wamempoteza mtu mahiri katika fani ya sheria kote visiwani na bara na mpigania haki za watu ndani na nje ya Tanzania. Profesa Haroub alikuwa mchangiaji mkubwa katika vipindi mbalimbali vya Sauti ya Amerika.

Zinazohusiana

XS
SM
MD
LG