Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 28, 2023 Local time: 20:09

Michael Jackson akumbukwa kote duniani


Mwana muziki mashuhuri kabisa wa muziki hapa Marekani Michael Jackson alifariki alhamisi tarehe 25 June baada ya kupatwa na mshtuko wa moyo nyumbani kwake huko Los Angeles. Alikua na umri wa miaka 50 na ni mmoja kati ya wasanii waliokua maarufu sana duniani ambaye alichanganya pamoja muziki wa aina ya pop, rock na soul uliowavutia watu wengi duniani wa kila rangi na utamaduni.

Michael Jackson alizaliwa tarehe 19 Augusti 1958 mjini Gary, Indiana akiwa mtoto wa saba kati ya watoto tisa. Yeye na kakazake wanne wakubwa walionekana tangu wadogo wakiwa na kipaji cha muziki, kuimba na kucheza dansa na hasa kuhimizwa na wazazi wao. Akiwa na umri wa miaka mitano alishuka kwa mara ya kwanza katika jukwaa na kuanza kuimba pamoja na ndugu zake hao wakiuwa na kundi la Jackson Five.

Baada ya mashindano ya muziki katika ukumbi mashuhuri wa Apollo huko New York Jackson Five walitia saini mkataba wao wa kwanza na kampuni ya rekodi ya Motown, na kuanzia 1964 hadi 1981 kwa pamoja ndugu hao waliuza zaidi ya rekodi milioni 100.

Mbali ya kuwa msanii hodari, mfanya biashara na mtu mkarimu Michael alikumbwa na kashfa kadhaa katika maisha yake na kubwa ni tuhuma ya kuwanajisi watoto wadogo, jambo ambalo mahakama iliamua hakua na hatia.

Kabla ya kufariki kwake, alikua anafanya mazoezi na matayarisho kwa ajili ya tamasha lake kubwa kabisa huko London la kutaka kurudi upya kwenye jukwaa la muziki na kuwaonyesha wakosowaji wake kwamba yungali ni mfalme wa pop. Lakini muda wake ulifika na aliaga dunia kwa ghafla kabisa. Mola amlaze pema Peponi.

XS
SM
MD
LG