Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 14, 2024 Local time: 23:10

Wanawake wabakwa jela Goma


Umoja wa Mataifa unaripoti kwamba zaidi ya wanawake ishirini walibakwa na wafungwa wanaume katika gereza kuu la mji wa Goma, mji mkuu wa jimbo la Kivu ya Kaskazini Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Afisi ya Umoja wa Mataifa huko Congo MONUC, imeleza hakuna mfungwa aliyeweza kutoroka kutoka jela hiyo. Wanawake 20 walibakwa na kuteswa na wafungwa hao ambao ni wanajeshi waliokua wamekamatwa kwa utovu nidhamu.

Akizungumza na sauti ya Amerika kutoka Goma, mtetezi wa haki za binadamu Bi Janine Bandu alisema alisikitika sana kuwaona wafungwa hao wa kike walivyoathirika. Alisema baada ya kubakwa na wafungwa wenzao, waliwekwa vyombo kwenye sehemu zao za uzazi na kupelekwa kwa matibabu katika hospitali za Goma.

Mtetezi huyo wa haki za binadamu anasema tatizo la ubakaji na manyanyaso dhdii ya wanawake limekuwa sugu, na kwamba mwanamke nchini Congo yumo katika hatari ya kubakwa wakati wowote ule. Bandu alikemea kitendo hicho kiovu na kuiomba serikali na wafadhili kutetea maslahi ya wanawake nchini humo.

Ripoti hiyo inaeleza kuwa afisa mmoja wa polisi aliuwawa pamoja na wafungwa watatu na walinzi wasiopungua tisa kuijeruhiwa baada ghasia hizo kuzuka katika gereza hilo.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi gereza hilo lilikuwa na wafungwa 837 ambapo 512 ni askari na wanajeshi wanaozuiliwa kutokana na makosa mbali mbali.

Umoja wa Mataifa umewataka wafungwa waliohusika na ghasia hizo na vitendo hivyo viovu waadhibiwe vikali na wakuu wa nchi wafanye mageuzi katika magereza yao pamoja na kuwatenga kabisa wafungwa wa kiume na wale wa kike.

XS
SM
MD
LG