Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 09, 2024 Local time: 12:59

Ali Kiba Azungumza na VOA


Hivi majuzi mwanamuziki wa muziki wa bongo flava - hasa kwa midundo yake ya chombeza - Ali Kiiba ambaye yuko hapa nchini Marekani kwa ziara ya maonyesho alitembelea studio zetu za Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika na kuzungumza na mtangazaji wa kipindi cha Burudani, Sunday Shomari.

Katika mahojiano hayo Ali Kiiba alizungumzia tangu alipoanzia muziki na alipofikia hivi sasa kama msanii maarufu sana Afrika Mashariki na Kati. Ali Kiiba anasema CD yake mpya tayari inapatikana katika maonyesho yake hapa Marekani na karibuni zitafika katika maduka ya muziki Afrika Mashariki na Kati. Sikiliza mahojiano kamili kati ya Sunday Shomari na Ali Kiiba.

XS
SM
MD
LG