Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 04:25

Ahmadinejad anapinga tuhuma za wizi wa kura


Rais wa Iran Mahamoud Ahmadinejad anasuta tuhuma za wizi wa kura katika uchaguzi wa rais ijumaa iliyopita, akisema alishinda mhula wa pili kutokana na uchaguzi huru.

Bw Ahmadinejad aliumnabia mkutano wawaandishi habari Jumapili kwamba kiwango chake cha ushindi katika uchaguzi huo wenye mabishano ni kikubwa kuweza kuwa na shaka yeyote. hapo baadae aliwashukuru maelfu wa wafuasi wake kwenye mkutano wa hadhara wa ushindi katika uwanja wa Vali Asr huko Teheran.

Matokeo rasmi yanaonesha kiongozi huyo wa kihafidhina amepata asili mia 63 za kura kulingana na asili mia 34 zakura alizopata mpinzani wake mpenda mageuzi Mir Hossein Mousavi.

Bw Mousavi ameituhumu serekali kwa wizi wa kura na kupinga matokeo hayo. Wafuasi wake walianda kwa siku ya pili mkutano wa malalamiko mjini Teheran siku ya Jumapili, wakitia moto matairi barabarani na kupambana na polisi.


XS
SM
MD
LG