Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:09

Ghailani adai Mahakamani NY, "Sina Hatia"


Maafisa wa wizara ya sheria ya Marekani wamemwasilishwa Mtanzania Ahmed Khalfan Ghailani mbele ya mahakama ya serekali kuu mjini New York na kufunguliwa mashtaka kwa kuhuiska kwake katika uripuaji wa mabomu kwenye ubalozi wa Marekani huko Kenya na Tanzania 1998.

Bw Ghailani alikamatwa nchini Pakistan mwaka 2004 na kuhamishwa na wafungwa wengine mwaka 2006 walotaja kua ni "wafungwa muhimu sana."

Maafisa wa wizara ya sheria wamefikisha mashtaka 286 dhidi ya Bw Ghailani ikiwa ni pamoja na kupanga njama pamoja na Osama Bin Laden na wanachama wengine wa al-Qaida ili kuwauwa Wamarekani, pamoja na mashtaka binafsi ya mauwaji ya kila aliyefariki katika mashambuliyo hayo ya mabomu.

Bw Ghailani amedai mbele ya hakimu kwamba hana hatia kufatana na tuhuma hizo zote.

Bw Ghailani ni mfungwa wa kwanza wa Guantanamo kufikishwa mbele ya mahakama ya kiraia hapa Marekani. Kesi yake inatazamiwa kua mtihani wa kwanza muhimu kwa mpango wa Rais Barack Obama wa kulifunga gereza la Guantanamo mnamo miezi saba ijayo, na kuwafikisha wafungwa mahakamani.

XS
SM
MD
LG