Rais omar Bongo alifariki akiwa na umri wa miaka 73 baada ya kugua kwa muda katika zahanati moja huko Barcelona, Hispania, kutokana na kile serekali ya Gabon inaeleza ni "mshtuko mkubwa" kufuatia kifo cha mkewe mwezi March mwaka huu.
Kifo chake na ugonjwa wake hapo kabla zilizusha ripoti za kutatanisha, ambapo vyombo vya habari viliripoti awali kwamba amelazwa hospitali akiwa mahtut kutokana na ugonjwa wa saratani ya tenzi kibofu, serekali ikikanusha. Na shirika la habari la Ufaransa liliporipoti kifo chake Jumapili tarehe 7 June serekali ikakanusha.
Rais Bongo alichukua madaraka 1967 akiwa wakati huo kiongozi kijana kabisa aktika bara la Afrika. Alichukua madaraka baada ya kifo cha rais Leon M'ba aliyefariki miaka 7 baada ya kuchukua madaraka kutoka ukoloni wa Ufransa.
Wakati wote wa utawala wake alijaribu kua mpatanishi wa migogoro ya nchi mbali mbali ya afrika ikiwa ni pamoja na Jamhuri ya Afrika ya Kati, Burundi , Na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongol. Lakini Gabon ilikua nchi ya pili ya Afrika iliyotambua uhuru wa walotaka kujitenga huko Biafra nchini Nigeria.
Kiongozi huyo wa muda mrefu, aliyesilimu mwaka 1973 na kubadilisha jina lake la Albert Bernad Bongo na kua Omar Bongo, alikubali mfumo wa vyama vingi mwaka 1990, lakini aliendelea kutumia utawala wa mabavu hadi kufariki kwake.
Yeye ni mmoja kati ya viongozi watatu wa Afrika wanaofanyiwa uchunguzi na jaji mmoja wa Ufaransa kwa mashtaka ya ulaji rushwa na utumiaji mbaya wa fedha za umaa. Shirika la kimataifa la kupambana na ulaji rushwa Tranparency International inadia zaidi ya nyumba na majengo ya familia ya Bongo huko Ufarnsa yanthamani ya zaidi ya dola milioni 200.