Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 07, 2023 Local time: 01:48

Obama Ziarani Mashariki ya Kati


Rais wa Marekani Barack Obama amepokelewa kwa heshima kamili za kiongozi kwa gwaride la kijeshi na viongozi wote wa serekali ya Saudi Arabia wakiongozwa na mfalme Abdullah huko Riyadh.

Alipowasili Bw Obama akasifu uhusiano muhimu na historia ya urafiki wa muda mrefu kati ya nchi zao mbili. Alisema amewasili mahala Uislamu ulianza ili kushauriana na mfalme wa Saudia juu ya masuala yanayoikabili mashariki ya kati.

Viongozi hao wawili wakaelekea kwenye shamba la mfalme kwa mazungumzo ya faragha juu ya ugomvi wa Israel na Palestina, jukumu la Iran katika eneo hilo na bei za mafuta duniani.

Rais wa Marekani ataelekea Misri kesho kutoa hotuba inayosubiriwa kwa muda mrefu kwa jumuia ya kislamu, ambayo itazungumzia juu ya utaratibu wa Mashariki ya Kati na masuala ya siasa kali za kidini na ghasia.

Huko Misri wanajitayarisha kumpokea Rais Obama na wakimchukulia kua mtu ambae huwenda atakua na fimbo la uchawi kutanzua mzozo wa Mashariki ya Kati kama anavyoeleza mwandishi habari Ismael Mfaoume huko Cairo.

Zinazohusiana

XS
SM
MD
LG