Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 22:50

Wakenya Wazomea Hotuba ya Rais Kibaki


Hotuba ya Rais Mwai Kibaki wa Kenya ilikatishwa kwa kelele za wananchi waliokuwa kwenye mkutano wa kuadhimisha miaka 46 tangu nchi hiyo ilipojipatia uhuru wake wa ndani.

Katika hali ya kuashiria kuwa hawaridhishwi na jinsi mambo yanavyo endelea nchini Kenya, wananchi walipiga kelele kumzomea Rais Kibaki pale alipokuwa akijaribu kuelezea mafanikio yaliyofikiwa nchini humo, na mikakati ya serikali yake kwa siku za baadaye.

Sarah Nyamvula ni mtetezi wa haki za mama na mtoto nchini Kenya. Anasema licha ya kwamba wakenya walijipatia utawala wao binafsi miaka 46 iliyopita, bado kuna ukiukwaji mkubwa wa haki za watoto, kina mama na binadamu wote kwa ujumla.

Naye mchambuzi wa siasa Maur Bwanamaka alisema kuwa Kenya imeharibika kwa sababu viongozi wa kisiasa wanazingatia zaidi malumbano ya kisiasa, na kwamba mwananchi wa Kenya bado anaendelea kunyanyasika licha ya kujipatia uhuru wake wa ndani miaka 46 iliyopita.

XS
SM
MD
LG