Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 24, 2024 Local time: 03:03

Raila: Uongozi Mbaya Unachelewesha Maendeleo Afrika


Akiongea na Sauti ya Amerika muda mfupi kabla ya kutoa hotuba yake katika chuo kikuu cha Buffalo, New York, Waziri Mkuu Odinga alisema kuwa mfumo mbaya wa uongozi umewanyima Waafrika haki ya kupanga namna ya kujiletea maendeleo yao wenyewe.

Bwana Odinga alisema kuwa Afrika inahitaji mabadiliko yatakayo saidia kupunguza mamlaka kupita kiasi yaliyowekwa katika taasisi za urais. Alisema hili litasaidia kuondokana na mifumo ya kidikteta, na kuingia mfumo wa uongozi wa kidemokrasia utakao wapatia mamlaka wananchi.

Akizungumza kuhusu suala la rushwa na mvutano wa kisiasa katika serikali ya mseto ya Kenya, Waziri Mkuu Odinga alisema kuwa tayari kuna maendeleo yaliyo patikana tangu ilipoundwa serikali ya mseto.

Hatahivyo, Bwana Odinga alikiri kuwa kumekuwepo na matatizo kadhaa katika serikali hiyo, lakini pia akasema mabadiliko tayari yanafanyika.

Alitoa mfano wa tume mpya ya uchaguzi ambayo imeundwa hivi karibuni, na kwamba Kenya iko katika harakati za kuunda tume ya ukweli, kaki na maridhiano itakayo saidia kuponya vidonda vilivyo patikana wakati wa machafuko yaliyofuatia uchaguzi wa nchi hiyo.

Zinazohusiana

XS
SM
MD
LG