Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Julai 24, 2024 Local time: 21:36

BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI LATOA MSAADA KWA ALBINO BURUNDI


Wabunge wa jumuiya ya Afrika Mashariki wametoa msaada wa fedha kusaidia chama cha Maalbino wa Burundi katika jitihada zao za kupambana na ugumu wa maisha na hali yao ya kiafya walitoa kiasi cha fedha sawa na faranga laki saba ili kuwasaidia maalbino hao baada ya mwakilishi wao ambaye ni mwenyekiti wa chama hicho Burundi kwenda kutoa hotuba kwenye kikao cha bunge hilo kinachoendelea huko Burundi. Mwenyekiti huyo wa chama cha maalbino amesema maalbino wengi wanakosa vitu muhimu ambavyo si vya gharama kama miwani na kofia na kudai kuwa wengi wao wanahitaji sana misaada aidha alielezea kuwa idadi yao kamili haijulikani na wanahitaji kujua idadi kamili. Ameelezea kuwa wengi wao bado wanaishi katika hali ya woga na maisha yao na kuitaka serikali kujihusisha zaidi na kuwasaidia zaidi.

Zinazohusiana

XS
SM
MD
LG