Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:44

UM Yalaani Jaribio la Nyuklia la Korea Kaskazini


Marekani, Russia, China na wanachama wengine 12 wa Baraza la Usalama, la Umoja wa Mataifa walikutana jana jioni katika kikao cha dharura, baada ya ulimwengu kupata habari za kushangaza kuhusu jaribio la nyuklia.

Mlipuko ulikuwa mkubwa kuwahi kufanywa na Korea Kaskazini, na ulifuatiwa na majaribio mengine matatu ya makombora aina ya ballistic.

Balozi Vitaly Churkin wa Russia, ambaye ni Rais wa sasa wa Baraza la Usalama alisema kuwa nchi zote zinapinga vikali vitendo vya Korea Kaskazini, na kukubaliana kwa pamoja kuitaka Korea Kaskazini iheshimu matakwa ya Umoja wa Mataifa.

Rais Barack Obama wa Marekani alisema program za nyuklia za Pyongyang ni kitisho kikubwa kwa amani na usalama kote duniani, na ukiukaji wa wazi wa sheria ya kimataifa.

XS
SM
MD
LG