Mshitakiwa wa kwanza wa kesi inayohusu ulipuaji mabomu balozi za Marekani nchini Tanzania na Kenya mwaka 1998, anatarajiwa kufikishwa mahakamani mjini New York.
Ahmed Kahlfan Ghailani, raia wa Tanzania ambaye amekuwa akishikiliwa katika gereza la Guantanamo Bay, Cuba anatuhumiwa kuhusika na ulipuaji huo wa mabomu na vifo vya watu zaidi ya 200.
Mama mzazi wa Ghailani, Bimkubwa Said Abdullah aliiambia Sauti ya Amerika kuwa angependa kuhudhuria kesi ya mwanae mara tu itakapoanza kusikilizwa mjini New.
Mkurugenzi wa upelelezi nchini Tanzania, Robert Manumba alisema kwa kuwa tukio la kigaidi lilitokea Tanzania mashahidi kadhaa wataondoka nchini humo kwenda New York kutoa ushahidi.