Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 10, 2023 Local time: 03:22

Somalia Yakanusha Kuingia tena Majeshi ya Ethiopia


Ripoti kutoka Somalia zinasema wanajeshi wa Ethiopia wamerudi nchini humo kujaribu kurejesha hali ya usalama baada ya waasi wa nchi hiyo kuzidisha mashambulizi katika mji mkuu wa nchi hiyo Mogadishu.

Lakini Waziri wa Habari wa Somalia Farhan Ali Mohamud anasema serekali imesikia ripoti hizo kutoka vyombo vya habari kuwa majeshi ya Ethopia yameingia lakini anasema hadhani ni ripoti sahihi.

Hatahivyo alisema inaeleweka kwa Ethopia kupeleka wanajeshi wake kwenye mpaka kujilinda kutokana na kuendelea kwa vita i upande wa pili wa mpaka ndani ya Somalia.

Majeshi ya Ethopia yaliondoka mwezi Januari mwaka huu baada ya makubaliano ya amani kufikiwa kati ya serekali na kundi la Rais Sharif Sheikh Ahmed katika upinzani, lakini Ethopia ilisema majeshi yatarudi ikiwa maslahi yake yako hatarini.

Ethopia ina kikosi kikubwa cha wanajeshi kwenye mpaka wake. Serekali ya Ethopia imekanusha kwamba wanajeshi wake wameingia nchini humo. Tangu May 8 wanaharakati kutoka makundi ya al-Shabab na Hizbul Islam, mungano wa wanamgambo wamekua wakipambana na majeshi ya serekali na wanamgambo wanaoiunga mkono serekali na majeshi ya kulinda amani ya Umoja wa Afrika.

XS
SM
MD
LG