Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 12:14

Walimu Waishitaki Serikali ya Tanzania


Chama cha walimu nchini Tanzania kimeishitaki serikali ya nchi hiyo kwa shirika la kazi duniani na shirika la kutetea haki za binadamu nchini humo baada ya walimu kushindwa kulipwa mishahara, baadhi yao tangu mwaka uliopita wa 2008.

Akiongea na Sauti ya Amerika kwa njia ya simu, msemaji wa walimu hao, Ezekaya Oluochi alisema Ijumaa kuwa walimu wamefanya kila linalowezekana kisheria kupata ufumbuzi wa tatizo lao bila mafanikio.

Bwana Oluochi alisema kuwa wameamua kuishitaki serikali kwa shirika la kazi duniani ILO na shirika la shirika la kutetea haki za binadamu nchini humo baada ya serikali kupuuzia kwa muda mrefu matatizo yao.

Naye Mwalimu Mtaita Neema kutoka Dar es Salaam, alisema kuwa amepoteza ari ya kufundisha baada ya serikali kukataa kumlipa mshahara wake tangu alipoanza kazi mwaka uliopita. Aidha amesema kuwa kwa sasa hatarudi shuleni hadi pale malipo yake yatakapo kuwa yametolewa.

XS
SM
MD
LG