Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 24, 2024 Local time: 11:00

Mabomu Mengine Yalipuka Tanzania


Mmoja wa waathiriwa wa mabomu hayo alikaririwa akisema, "Hali ngumu sana. Jana sisi walipotutangazia tukae hapa hapa, tukaamua kukaa hapa. Sasa yalipoanza kulipuka, kwakweli hakuna aliyekaa."

Aidha mama huyo alisema kuwa watu walikimbia huku na huko wakihofia maisha yao, na kwamba watoto wawili waliangukiwa na ukuta, na wengine walipata matatizo ya masikio. Maelezo hayo yaliungwa mkono na mama mwingine aliyetoa mwito kwa serikali kuwaondoa kwenye makazi yao ya muda kwa maelezo kuwa wanakabiliwa na hali ngumu.

Aidha wananchi hao wameeleza kuwa wanakabiliwa na tatizo la usalama baada ya kuona dalili za kuwepo watu wanaoweza kuwa na nia ya kuwavamia kwa lengo la kuiba vitu kidogo walivyo kimbia navyo.

Mwenyekiti wa chama cha upinzani nchini Tanzania, Profesa Ibrahim Lipumba ameitaka serikali kueleza bayana kinachoendelea huko Mbagala.


Zinazohusiana

XS
SM
MD
LG