Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 07, 2024 Local time: 11:02

Mgogoro wa Migingo Waingia Sura Mpya


Rais Yoweri Museveni alikaririwa akisema kuwa amekasirishwa na jamii ya wajaruo nchini Kenya ambao anasema kuwa wana wazimu.

Bwana Museveni alisema kuwa tatizo la kisiwa cha Migingo ni dogo mno kiasi kwamba halistahili kuleta uhasama kati ya nchi hizo mbili. Amesema kama Uganda ikizingatia kwa makini, sheria iliyopo, hakuna mvuvi kutoka Kenya ataruhusiwa kuvua samaki katika kisiwa hicho.

Alisema kuwa mara kwa mara amekuwa akishauri jamii ya wajaruo wa Kenya ambao wamekuwa wakifanya uharifu wa kung'oa reli inayoziunganisha nchi hizo mbili na kufanya maandamano kuwa hakuna mvuvi kutoka Kenya atakaye ruhusiwa kuvua samaki katika maji ya kisiwa hicho.

Kutokana na msimamo huo wa Rais Museveni, baadhi ya wabunge katika jimbo la Nyanza nchini Kenya wameanza kulalamika kuhusu matamshi hayo ya Rais Museveni. Wabunge hao wamemtaka Rais Kibaki kupeleka wanajeshi wa Kenya katika kisiwa hicho, na na wametishia kuchukua sheria mikononi mwao kama Rais Kibaki atashindwa kufanya hivyo.

Zinazohusiana

XS
SM
MD
LG