Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 14, 2024 Local time: 12:41

Serikali ya mseto Kenya bado yavutana 


Serikali ya Kenya inaendelea kukabiliwa na migogoro ya kisiasa huku kukiwa na mvutano kati ya vyama vikuu vya serikali hiyo ya mseto. Wakenya wengi wameanza kusema ilikuwa bora nyakati za kulikuwa na utawala wa rais na makamu wa rais na kwamba serikali ya sasa haishughulikii masuala yao kutokana na mvutano baina ya vyama hivyo. Itakumbukwa kwamba tangu serikali ya mseto kuingia madarakani kumekuwa na malumbano ya juu ya nani ni kiongozi wa shughuli za serikali bungeni na vile vile tofauti kati ya rais Kibaki na mawaziri wake zilipelekea kujiuzulu kwa waziri wa sheria Martha Karua. Sasa baadhi ya wananchi wa Kenya nao wametoa duku duku lao juu ya tofauti hizi. Mwanasheria na mchambuzi wa masuala ya kisiasa wa Kenya P.L.O Lumumba akizungumza na sauti ya Amerika anasema "kiti hiki cha waziri mkuu hakifai wala hatukihitaji kwani tangu kumekuwa na wadhifa huu imekuwa ni migogoro na migongano". Alielezea msimamo wake juu ya sakata hili na kutoa mawazo yake juu ya uchaguzi nchini humo katika mahojiano na sauti ya Amerika.

XS
SM
MD
LG