Ajali hiyo ilitokea mapema Jumatatu wakati Kamishna mkuu wa jeshi la polisi nchini Kenya, Meja Jenerali Hussein Ali, pamoja, waziri msaidizi wa usalama wa Taifa Bwana Ejode, na mkuu wa mkoa wa Rift Valle, walipokuwa wakisafiri ndani ya ndege hoyo wakati ndege hiyo ilipoishiwa nguvu na kuanguka.
Hakuna taarifa za vifo zilizopatikana mara moja, lakini iliripotiwa kuwa abiria kumi walijeruhiwa na wengine kadhaa kupelekwa katika hospitali ya Eldoret kwa matibatu. Majeruhi wawili kati ya hao walijeruhiwa vibaya sana.
Watu walioshuhudia ajali hiyo, wanasema ndege hiyo ambayo ni helkopta ya polisi, iliharibika sana baada ya kuanguka. Ndege hiyo ni miongoni mwa ndege zilizokuwa zimewabeba maafisa wa usalama waliokuwa safarini kukagua hali ya usalama katika eneo hilo.