Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 03, 2023 Local time: 05:12

Hakuna Jipya Kutoka kwa Kilonzo


Akiongea na Sauti ya Amerika Kutoka Nairobi, mchambuzi wa siasa PLO Lumumba alisema Jumatatu kuwa wakenya wasitegemee mabadiliko mapya kutoka kwa waziri mpya Mutula Kilonzo, na kwamba yeyote ambaye angechaguliwa kushika nafasi hiyo asingeweza kuleta mabadiliko yoyote.

Bwana Lumumba alisema kuwa kitu cha muhimu kwa sasa ni kufanya mabadiliko ya katiba. Lakini alisema kuwa swala hilo bado halijapewa kipa umbele na tume husika, na kwamba hata wananchi wa kawaida hawana msisimko wa kutaka mabadiliko hayo.

Alionya kuwa kama wakenya wasipo chukua tahadhari katika kushughulikia suala hilo, kuna hatari kuwa zitaundwa nyadhifa zisizofaa kati ya chama cha ODM na PNU. Alikumbusha kuwa wananchi wa Kenya wanahitaji katiba itakayo wasaidia kupata bunge linalofaa na ambalo litashughulikia kikamilifu mahitaji yao.

Zinazohusiana

XS
SM
MD
LG